Tamwa: Vyombo vya habari vimeleta mabadiliko nchini
“Tumeridhishwa na michango yenu, nyie wahariri pamoja na waandishi wa habari za wanawake na watoto.
“Tunaona matatizo mengi katika jamii ya kuteswa na kunyanyapaliwa kwa watoto wa kike na wanawake kwa ujumla yamepungua ingawa kuna baadhi ya sehemu bado ukandamizaji upo lakini tuna imani kadiri jamii inavyopatiwa taarifa itazidi kuelewa na litapungua kama siyo kuisha kabisa,” alisema Msoka.
Aliwataka watunga sera kuhakikisha sheria za kulinda haki za wanawake zinazingatiwa na zinapoonyesha kuna upungufu zirekebishwe mapema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TAWLA), Tike Mwambipile aliiomba Serikali iwe na chombo au taasisi maalumu itakayojihusisha na masuala ya ijinsia tu.
Alisema katika kipindi hiki cha kutoa maoni ya Rasimu ya Katiba Mpya, inafaa wajitokeze kwa wingi kuzungumzia masuala wanayoyaona hayafai kuwekwa katika Katiba, kwa kufanya hivyo itakuwa njia mojawapo ya kupata kile wanachokitaka.
Kuhusu utawala bora, alisema wanawake wamekuwa wakinyanyaswa kwa kuombwa rushwa ya ngono kisha wapatiwe kile wanachokihitaji, hivyo amewaomba wasivumilie bali watoe taarifa katika vyombo vya habari na kwingineko kwa ajili ya kukomesha hali hiyo.
Chanzo: Gazeti la Mtanzania
No comments:
Post a Comment