MFUMO
Hazina wakwama kulipa
Toleo la 263
17 Oct 2012
- Ni pamoja na mishahara na madeni
- Wasema mifumo iliyopo inawaangusha
MFUMO wa malipo ya fedha kwa wanaoidai Serikali umekwama, Raia Mwema limebaini.
Na kwa sababu ya kukwama huko, wizara na taasisi mbalimbali nchini nazo zimekwama kuendesha baadhi ya shughuli zao, na hata kuchelewa kulipa mishahara ya wafanyakazi wao kwa wakati.
Ingawa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah, amethibitisha kuwapo kwa tatizo hilo akisema chanzo chake ni kuharibika kwa mfumo wa kompyuta Hazina (Intergrated Financial Systems), lakini zipo taarifa kwamba mfumo huo umechezewa makusudi kwa manufaa ya baadhi ya watendaji.
Taarifa zilizopo zinabainisha kwamba, mfumo huo ambao unatajwa kudhibiti mbinu za ukwapuaji fedha kwa njia ya malipo ambao umekuwa ukifanywa kati ya baadhi ya watendaji wa wizara au idara za Serikali na baadhi ya watendaji wa Hazina, umekuwa kikwazo kwa baadhi ya watendaji kufanya njama za ufisadi.
Ni kutokana na kuharibika kwa mfumo huo, vyanzo vyetu vya habari vinabainisha kwamba takriban miezi zaidi ya mitatu sasa baadhi ya malipo kwa watumishi serikalini hayakufanyika kwa wakati. Mbali na malipo hayo kwa wafanyakazi serikalini, hata malipo kwa wanaoidai Serikali kutokana na ‘kuiuzia’ huduma mbalimbali yamekuwa kitendawili kwa muda mrefu sasa.
Katika wizara na idara za Serikali, lawama zote zimekuwa zikielekezwa Hazina ambayo iko chini ya uongozi mpya wa Waziri Dk William Mgimwa na manaibu waziri wawili, Janeth Mbene na Saada Mkuya Salumu.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, michakato ya malipo kama vile mishahara ya wafanyakazi, imekuwa ikifanyika kwa wakati na kuwasilishwa Hazina kwa ajili ya mchakato wa ulipaji wa fedha.
“Mimi mwenyewe sijalipwa kwa miezi kadhaa sasa baadhi ya malipo yangu. Tayari ofisini yamekwishaidhinishwa na kupitia mchakato wote, lakini ni miezi kadhaa sasa sijalipwa. Tatizo ni Hazina, wanachelewesha malipo,” kilieleza chanzo chetu cha habari ndani ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
Akizungumza na mwandishi wetu kuhusu tatizo hilo na lawama zinazoelekezwa Hazina , Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Kijjah, alisema: “Ni kweli kumekuwa na tatizo hilo na juhudi zimefanyika kulitatua.”
Kwa mujibu wa Kijjah, kilichotokea ni kuharibika kwa mfumo wa taarifa na takwimu za kifedha, ambao kwa kifupi unajulikana kama IFS ambao unatumia teknolojia maalumu ya kompyuta.
“Malipo siku hizi yanafanyika katika michakato ya aina mbili. Kuna mchakato wa kawaida ambao baada ya kukamilishwa, unaingizwe kwenye mchakato wa pili wa kuweka katika Intergrated Financial Systems (IFS). Tulichokwama ni kwenye IFS, mfumo wetu umeharibika na tumepata watalaamu kutoka kampuni ya Softech,” alisema Kijjah.
Katika maelezo yake kwa mwandishi wetu, Katibu Mkuu huyo wa Hazina, alisema hitilafu hiyo ya kimfumo imetokana na tatizo la umeme wakati mwingine kuzidi na wakati mwingine kupungua nguvu.
“Mfumo umeharibika kwa sababu ya umeme. Unajua umeme wetu wakati mwingine unakuwa na matatizo. Sasa tatizo limechukua muda kwa sababu mwanzo hakutukuwa na timu ya ufundi ya kusimamia mfumo huu. Baada ya kufungwa ikawa basi, kwa sasa tumewapa kazi Softech. Wanarekebisha pamoja na kusimamia mfumo huo ili ufanye kazi vizuri wakati wote,” alisema Kija.
Hali hiyo inajitokeza katika wakati ambao Wizara ya Fedha imepata kulalamikiwa na baadhi ya mawaziri kutowasilisha fedha za bajeti kwa wizara nyingine kama Bunge linavyoidhinisha.
Kati ya mawaziri waliopata kulalamika wizara zao kupewa fedha pungufu ya bajeti inayopitishwa na Bunge ni pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Katika hotuba yake ya makadirio ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alilalamika bungeni akisema wizara yake ilipewa asilimia 44 tu ya bajeti iliyopitishwa mwaka uliopita wa kibajeti.
Membe alisema; “Wizara yangu imeendelea kupata mgao kidogo sana wa bajeti isiyokidhi mahitaji katika mwaka wa fedha 2011/2012. Katika kipindi tajwa, Wizara yangu ilipata asilimia 44 tu ya Bajeti iliyoombwa. Bajeti ndogo tunayopewa imekuwa changamoto kubwa katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa kiwango kinachostahiki.”
Hata hivyo, Membe alisema pamoja na kasoro hizo za kibajeti, wizara hiyo kwa nafasi yake kama kiungo muhimu kati ya Tanzania na nchi za nje, imeendelea kushirikiana kwa karibu na wizara, idara na taasisi mbalimbali za serikali pamoja na sekta binafsi ili nchi ifaidi fursa mbalimbali katika sekta za uchumi na jamii.
Katika hatua nyingine, kitendo cha Wizara ya Fedha kulalamikiwa kila mara kinamweka katika wakati mgumu Waziri (mpya) wa Fedha, Dk. Mgimwa, ambaye kwa sasa mawaziri wengine wenzake wameonekana kuongeza kasi ya ufanisi katika wizara zao.
Mawaziri ambao kwa sasa wameongeza kasi ya ufanisi katika wizara zao ni pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ambaye anapambana kulinyoosha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.

No comments:
Post a Comment