Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Monday, September 16, 2013

Pembe Tatu ya Wazazi, Wanafunzi na Shule yaanza kujidhihirisha!

Wazazi watakiwa kuweka mkazo wa elimu

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga, Abdi Makange, amewataka wazazi na walezi mkoani hapa kuweka msukumo wa elimu kwa watoto wao. Kauli hiyo aliitoa mjini hapa hivi karibuni wakati wa Mahafali ya Shule ya Sekondari Mlongwema.
Alisema hakuna urithi muhimu hapa nchini zaidi ya elimu hivyo wazazi wanapaswa kulitilia mkazo suala hilo kwa umakini mkubwa.
Alisema endapo wanafunzi watasoma kwa bidii ikiwamo kuzingatia masomo itawasaidia kuweza kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho na kupata kazi nzuri itakayouwa dira katika kuendeleza maisha yao na jamii zao.
“Ukisoma utakuwa na amani ya moyo kwani unaweza kumu abudu Mungu kwa moyo mmoja bila kuweka mawazo ya wapi nitapata maisha mazuri, hivyo ndugu zao naombeni msome kwa bidii na matunda yake mtayaona,” alisema Makange.
Aliwataka wazazi kuwa mstari wa mbele kutoa michango muhimu inayohitajika kwa watoto wao iweze kuchangia kasi ya maendeleo katika shule hiyo.
Awali, akisoma risala, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, John Tembo, alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa vifaa vya sayansi na walimu kwa kuwa yupo mwalimu mmoja pamoja na uhaba wa nyumba wa walimu kwa kuwa zilizopo hazitoshelezi.

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts