Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Monday, September 16, 2013

Habari za Gazeti la Malawi ni Uzushi-Habari Maelezo.


Serikali: Hatukuwalenga wahamiaji wa Malawi

SERIKALI imesema mpango wa kuwarejesha wahamiaji haramu nchini kwao haukuilenga nchi yoyote, bali ni utaratibu wa kawaida wa kiutendaji na hautasitishwa kwa hofu ya kutukanwa na vyombo vya habari vya nchi husika. Aidha, imelitaka gazeti la Malawi News la Malawi kukanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti hilo kuwa Tanzania imeilenga nchi hiyo na katika mpango huo, Mmalawi mmoja alibakwa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene, alisema taarifa hizo si sahihi na gazeti hilo linapaswa kusahihisha taarifa hizo kabla Serikali haijalichukulia hatua za kisheria.
“Taarifa hizo zilizochapishwa na gazeti hilo la Septemba 14, mwaka huu, zinasema kuwa Tanzania imewanyanyasa, kuwatesa na kuwabaka Wamalawi wanaoishi nchini, jambo lililosababisha wengine waliosalia kujifungia ndani wakihofia usalama wao.
“Cha kusikitisha zaidi ni kwamba taarifa hizo zimethibitishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi pamoja na ubalozi wake nchini.
“Ukweli ni kwamba, Serikali haijailenga Malawi katika mpango huu, Wamalawi wanaoishi nchini ni mashahidi kwa kuwa walikamatwa 1,030, wakahojiwa na Idara ya Uhamiaji Mkoa.
“Wote walionyesha nia ya kuishi nchini, wakapewa fomu za kujaza na wameruhusiwa kuishi nchini, hakuna Mmalawi aliyekamatwa, kunyanyaswa, kuteswa wala kubakwa, isipokuwa wanafanya taratibu za kuhalalisha ukaazi wao,” alisema Mwambene.
Alisema Serikali inashangazwa na taarifa hizo, kwa kuwa pamoja na kuwafanyia hisani watu wake, gazeti hilo limeitukana.
Alisema ni aibu kwa chombo kikubwa cha habari kama hicho kutoa taarifa hizo kwa kuwa mpango huo sio siri na Rais Jakaya Kikwete alishatangaza na kutoa wiki mbili kwa wahamiaji wote haramu kuomba kibali cha kuishi nchini au kuondoka kwa hiyari.
Akizungumzia utaratibu wa kuwashitaki wahamiaji hao haramu, alisema suala hilo lina ugumu kutokana na wingi wa wahamiaji hao zaidi ya 25,000 na kwamba uendeshaji wa kesi hizo utachukua muda mrefu.
“Labda wa kulalamika wangekuwa watu wa Rwanda na Burundi ambao ndiyo wengi, Burundi pekee ina wahamiaji 12,000 na Rwanda 6,000, ikifuatiwa na nchi za Congo, Zambia na Malawi yenyewe.
“Lakini hatujapata malalamiko kutoka kwa nchi nyingine, sheria ziko wazi, ukikamatwa unaishi kinyume cha sheria unatakiwa uondoke kwa sababu unahatarisha usalama wa wananchi waliopo,” alisema Mwambene.
Katika hatua nyingine, wahamiaji haramu 6,809 wamekamatwa katika kipindi cha siku 10 tangu Oparesheni Kimbunga ianze katika Mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma.
Wahamiaji hao kati yao ni raia 1,446 wa Rwanda, 4,229 wa Burundi, 647 wa Uganda, 443 wa Kongo, 42 wa Somalia, India na Yemen mmoja mmoja.
Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro, alisema hayo jana wakati akizungumzia operesheni hiyo inavyoendelea tangu ilipoanza Septemba 6, 2013.
“Wahamiaji walioondoka kwa hiyari ni 1,866, walioachiwa huru 396, walioondoka kwa agizo la Mahakama 2,377 na 2,170 wanaendelea kuhojiwa,” alisema.
Chanzo: Gazeti Mtanzania

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts