Uchunguzi waitia hatiani polisi, jeshi kwenye ghasia za Tana River
Septemba 20, 2013
Uchunguzi juu ya ghasia za kikabila kati ya jamii za Wapokomo na Waorma kwenye eneo la Tana River Delta nchini Kenya
ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita umewatia hatiani askari na
wanajeshi wastaafu, liliripoti gazeti la The Standard la Kenya siku ya
Alhamisi (tarehe 19 Septemba).
Ripoti hiyo inatoa tuhuma kwamba maafisa wa usalama walitoa silaha, sare za kijeshi, taarifa za kijasusi na mafunzo kwa watu wa makabila yao.
Uchunguzi huo pia uligundua kwamba wanachama wa kundi la Baraza la Jamhuri ya Mombasa wanaopigania kujitenga kwa mkoa wa pwani na wa al-Shabaab walishiriki kwenye ghasia hizo.
"Mashambulizi haya yalifanywa na makundi ya uhalifu wa kupanga katika namna ya mpangilio mkubwa kabisa na kukiwa na aina fulani ya muundo wa amri. Mashambulizi yenyewe yalifanywa kwa mbinu za kijeshi, hali inayoonesha kwamba makundi hayo yalikuwa yamepata mafunzo kabla ya mashambulizi hayo," ilisema ripoti hiyo.
Zaidi ya watu 170 waliuawa na kiasi cha 10,000 kulazimishwa kuyahama makaazi yao katika mfululizo wa ghasia kutoka mwezi Agosti 2012 hadi mwanzoni mwa mwaka 2013 zilizohusishwa na migogoro ya kikabila juu ya radhi, maji na nguvu za kisiasa.
Chanzo: Sabahionline

No comments:
Post a Comment