Mahakama inayohamishika ya Usalama barabarani nchini Kenya yadhamiria kupunguza ajali
Na Rajab Ramah, Nairobi
Septemba 19, 2013
Mfumo mpya wa Kenya wa mahakama zinazohamishika za usalama
barabarani, ambapo mahakimu hujadili na kuwaadhibu waendesha magari
wanaovunja sheria katika mahema, unapunguza idadi ya ajali za barabarani
nchi nzima, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Usalama barabarani
Samuel Kimaru.
Tangu programu hiyo ilipozinduliwa tarehe 22 Agosti, maofisa wa polisi wamekuwa wakiwakamata madereva wanaotuhumiwa kuendesha kwa kasi au kwa uzembe na kukagua magari katika vituo vya ukaguzi, wakati ambapo mahakimu wanasikiliza kesi kwa muda katika vyumba vya mahakama sehemu iliyo jirani.
Mahakama zinazohamishika za usalama barabarani ni sehemu ya kampeni ya serikali ya "Usalama Kwanza" ili kupunguza viwango vya vifo vinavyohusiana na ajali za barabarani nchini Kenya.
"Bado hatujafanya utafiti wa idadi, lakini kwa makisio yangu, ajali zimepungua kwa asilimia 50," Kimaru aliiambia Sabahi.
Takwimu za polisi wa usalama barabarani zinaonesha kwamba wastani wa Wakenya 3,000 hufa kila mwaka katika kupinduka na ajali nyingine za barabarani, Kimaru alisema.
Kwa mujibu wa Wizara ya Usafirishaji na Miundombinu ya Kenya, kuanzia Januari hadi katikati ya Julai, Wakenya 1,725 walikufa katika ajali za barabarani -- watembea kwa miguu 796, abiria 442, waendesha pikipiki 170, madereva 161, waendesha baisikeli 77 na abiria wa baisikeli 79.
"Tangu tulipoanza [programu] majuma matatu yaliyopita, tunaona utambuzi kiasi upande wa waendesha magari katika namna ambayo wanatumia barabara zetu," Kimaru alisema, akiongeza kwamba hivi karibuni operesheni itapanuliwa.
Hata hivyo, Kimaru na viongozi wengine wa polisi walikosolewa baada ya basi lililopinduka huko Narok kuua watu wapatao 41 mwishoni mwa Agosti.
Chama cha Jamii ya Sheria cha Kenya ilimkosoa Kimaru kwa kushindwa kutekeleza sheria za barabarani na kumpa muda hadi mwishoni mwa Septemba kuja na "mpango kazi wa kuaminika na wa kushawishi" ili kuboresha usalama wa barabarani.
Kimaru alikiri kwamba kuna baadhi ya matatizo katika mfumo mpya.
Baadhi ya wenye magari wanavunja sheria kwa kutumia njia ya mzunguko wanapoona polisi wamejipanga katika vituo vya ukaguzi katika njia zao, alisema.
"Tunafanyia kazi taratibu za jinsi kila ofisa wa polisi nchini atakavyotumika kutimiza sheria za barabarani," alisema. "Hivyo kwa jinsi tunavyoongeza uwezo wa kushughulikia suala hili kikamilifu, [tunafanya] vigumu kwa waendeshaji kuepuka majarife yetu."
Uvunjaji wa sheria kwa mara ya kwanza unaagizwa kulipa faini, wakati wale wenye makosa ya awali wanapelekwa jela, alisema Kimaru. Abiria ambao hawakufunga mikanda ya usalama pia wanakabiliwa na faini na ikitokea gari halina mikanda ya usalama mmiliki hushtakiwa pia.
Faini kwa uvunjaji wa baadhi yasheria za barabarani zinaweza kuwa kati ya shilingi 10,000 (dola 114) hadi 50,000 (dola 571), kwa mujibu wa Kimaru.
Mahakama zinazohamishika pia zinafanya kazi kupunguza hongo na rushwa kwa polisi, kwa mujibu wa Polisi Inspekta Generali David Kimaiyo.
Maofisa wa tume wanakwenda bila kujulikana katika mahakama zinazohamishika kuhakikisha kwamba waajiriwa wa serikalini hawapokei hongo, aliiambia Sabahi.
"Hadi sasa tumewabadilisha vituo makamanda tisa na wengine zaidi ya 200 wataathirika," alisema Kimaiyo. "Kwa wale waliokuwa wakitoroka kwa tuhuma za ufisadi, tuna maofisa kutoka katika Tume ya Maadili na Kuzuia Rushwa wakiwachunguza. Kama watapatikana na makosa, tutawafukuza na kuwaacha wakabiliane na sheria."
Mfanyabiashara wa mtaani wa Nairobi Simon Ayuma, mwenye umri wa miaka 32, alipongeza upande wa mahakama za makosa ya barabarani.
"Hili ni wazo zuri ambalo litasaidia kuondoa madereva wasiokuwa na akili timamu na magari yasiyofaa katika barabara zetu," alisema. "Madereva hawa katili wametufanya sisi kuwakosa ndugu zetu, [lakini] kupitia jitihada hizo, usalama wa barabara zetu unaweza kuhakikishwa."
Bado mambo mengi yanatakiwa kufanywa kuzuia kiwango kikubwa cha ajali za barabarani, kama vile kujenga barabara nzuri na kuweka alama za barabarani, alisema Samuel Mutiso, mwenye umri wa miaka 50, mwalimu wa shule ya upili mjini Nairobi.
"Tunapaswa pia kufunga kamera katika barabara kuu zote ili wavunjaji wa sheria za barabarani waweze kuonekana wakati wowote na kushtakiwa," alisema.
Chanzo: Sabahionline
Tangu programu hiyo ilipozinduliwa tarehe 22 Agosti, maofisa wa polisi wamekuwa wakiwakamata madereva wanaotuhumiwa kuendesha kwa kasi au kwa uzembe na kukagua magari katika vituo vya ukaguzi, wakati ambapo mahakimu wanasikiliza kesi kwa muda katika vyumba vya mahakama sehemu iliyo jirani.
Mahakama zinazohamishika za usalama barabarani ni sehemu ya kampeni ya serikali ya "Usalama Kwanza" ili kupunguza viwango vya vifo vinavyohusiana na ajali za barabarani nchini Kenya.
"Bado hatujafanya utafiti wa idadi, lakini kwa makisio yangu, ajali zimepungua kwa asilimia 50," Kimaru aliiambia Sabahi.
Takwimu za polisi wa usalama barabarani zinaonesha kwamba wastani wa Wakenya 3,000 hufa kila mwaka katika kupinduka na ajali nyingine za barabarani, Kimaru alisema.
Kwa mujibu wa Wizara ya Usafirishaji na Miundombinu ya Kenya, kuanzia Januari hadi katikati ya Julai, Wakenya 1,725 walikufa katika ajali za barabarani -- watembea kwa miguu 796, abiria 442, waendesha pikipiki 170, madereva 161, waendesha baisikeli 77 na abiria wa baisikeli 79.
"Tangu tulipoanza [programu] majuma matatu yaliyopita, tunaona utambuzi kiasi upande wa waendesha magari katika namna ambayo wanatumia barabara zetu," Kimaru alisema, akiongeza kwamba hivi karibuni operesheni itapanuliwa.
Hata hivyo, Kimaru na viongozi wengine wa polisi walikosolewa baada ya basi lililopinduka huko Narok kuua watu wapatao 41 mwishoni mwa Agosti.
Chama cha Jamii ya Sheria cha Kenya ilimkosoa Kimaru kwa kushindwa kutekeleza sheria za barabarani na kumpa muda hadi mwishoni mwa Septemba kuja na "mpango kazi wa kuaminika na wa kushawishi" ili kuboresha usalama wa barabarani.
Kimaru alikiri kwamba kuna baadhi ya matatizo katika mfumo mpya.
Baadhi ya wenye magari wanavunja sheria kwa kutumia njia ya mzunguko wanapoona polisi wamejipanga katika vituo vya ukaguzi katika njia zao, alisema.
"Tunafanyia kazi taratibu za jinsi kila ofisa wa polisi nchini atakavyotumika kutimiza sheria za barabarani," alisema. "Hivyo kwa jinsi tunavyoongeza uwezo wa kushughulikia suala hili kikamilifu, [tunafanya] vigumu kwa waendeshaji kuepuka majarife yetu."
Mahakama zaadhibu wanaovunja sheria, kupambana na rushwa
Viongozi wa usalama wanakamata magari yaliyopatwa yakivunja sheria za usalama na kutoa tiketi kwa wenye magari wanaoendesha kwa mwendo kasi au wasiokuwa na leseni.Uvunjaji wa sheria kwa mara ya kwanza unaagizwa kulipa faini, wakati wale wenye makosa ya awali wanapelekwa jela, alisema Kimaru. Abiria ambao hawakufunga mikanda ya usalama pia wanakabiliwa na faini na ikitokea gari halina mikanda ya usalama mmiliki hushtakiwa pia.
Faini kwa uvunjaji wa baadhi yasheria za barabarani zinaweza kuwa kati ya shilingi 10,000 (dola 114) hadi 50,000 (dola 571), kwa mujibu wa Kimaru.
Mahakama zinazohamishika pia zinafanya kazi kupunguza hongo na rushwa kwa polisi, kwa mujibu wa Polisi Inspekta Generali David Kimaiyo.
Maofisa wa tume wanakwenda bila kujulikana katika mahakama zinazohamishika kuhakikisha kwamba waajiriwa wa serikalini hawapokei hongo, aliiambia Sabahi.
"Hadi sasa tumewabadilisha vituo makamanda tisa na wengine zaidi ya 200 wataathirika," alisema Kimaiyo. "Kwa wale waliokuwa wakitoroka kwa tuhuma za ufisadi, tuna maofisa kutoka katika Tume ya Maadili na Kuzuia Rushwa wakiwachunguza. Kama watapatikana na makosa, tutawafukuza na kuwaacha wakabiliane na sheria."
Mfanyabiashara wa mtaani wa Nairobi Simon Ayuma, mwenye umri wa miaka 32, alipongeza upande wa mahakama za makosa ya barabarani.
"Hili ni wazo zuri ambalo litasaidia kuondoa madereva wasiokuwa na akili timamu na magari yasiyofaa katika barabara zetu," alisema. "Madereva hawa katili wametufanya sisi kuwakosa ndugu zetu, [lakini] kupitia jitihada hizo, usalama wa barabara zetu unaweza kuhakikishwa."
Bado mambo mengi yanatakiwa kufanywa kuzuia kiwango kikubwa cha ajali za barabarani, kama vile kujenga barabara nzuri na kuweka alama za barabarani, alisema Samuel Mutiso, mwenye umri wa miaka 50, mwalimu wa shule ya upili mjini Nairobi.
"Tunapaswa pia kufunga kamera katika barabara kuu zote ili wavunjaji wa sheria za barabarani waweze kuonekana wakati wowote na kushtakiwa," alisema.
Chanzo: Sabahionline
No comments:
Post a Comment