Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Saturday, September 14, 2013

Sheria Mpya Dawa za Kulevya Zifanyiwe Kazi, Siyo Kutunga tu.


Sheria ya dawa za kulevya kusukwa upya

SERIKALI inakusudia kuifanyia marekebisho sheria ya kudhibiti dawa za kulevya ya mwaka 1995, ili kuongeza kasi ya kukabiliana na tatizo hilo. Hatua hiyo inakuja baada ya Serikali kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kuweza kuifuta sheria hiyo na kutunga sheria mpya, itakayosaidia kuzuia mianya yote inayochochea tatizo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema sheria iliyopo sasa ina upungufu mkubwa.
Lukuvi, ambaye pia ni Mbunge wa Isimani, alisema upungufu huo unakwamisha jitihada za udhibiti na wakati mwingine watuhumiwa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wamekuwa wakishinda kesi zao mahakamani na kuleta hisia mbaya kwa jamii.
“Tunataka kutunga sheria mpya ya kupambana na madawa ya kulevya, ambayo inayotumika sasa ina mapungufu, pia tunataka kuanzisha chombo maalumu ambacho kitakuwa na mamlaka ya kisheria ya uchunguzi, kukamata na kupekua, ambacho kitakuwa na uwezo huo kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) isiyoingiliwa na chombo kingine.”
Alisema sheria hiyo imekuwa ikitoa adhabu isiyoendana na ukubwa wa makosa husika, jambo linalochochea kuendelea kushamiri kwa biashara ya dawa za kulevya.
“Mfano kifungu cha 21 kinachowahusu wafadhili wa biashara haramu ya dawa za kulevya, kinatoa adhabu ndogo ambayo wanaomiliki biashara hii wanakuwa na uwezo wa kulipa faini.
“Adhabu iliyopo ni faini ya shilingi milioni kumi au kifungo cha maisha, lakini adhabu hizi haziendi pamoja, inampa uhuru jaji au hakimu kutoa maamuzi ya kifungo au faini,” alisema.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema watuhumiwa wa makosa hayo wamekuwa wakifikishwa mahakamani bila ushahidi na baadaye kuachiwa.
“Kama tukimkamata mtu anafanya biashara ya dawa za kulevya na kukosa kidhibiti, tunampeleka mahakamani anakuwa chini ya uangalizi wa polisi na mahakama kwa miaka mitatu au mitano, kutegemeana na mahakama itakavyoona,” alisema. Chanzo: Mtanzania Gazeti

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts