Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Saturday, September 14, 2013

Tabia za Kumwagiana Tindikali ni Hatari!


Padri amwagiwa tindikali Zanzibar

PADRI wa Kanisa Katoliki Parokia ya Machui visiwani Zanzibar, Joseph Monesmo Mwang’amba (60), amejeruhiwa vibaya baada ya kumwagiwa maji yanayodhaniwa kuwa ni tindikali. Kiongozi huyo wa kidini, amemwagiwa maji hayo na watu wasiojulikana na kujeruhiwa katika sehemu mbali mbali za mwili hasa usoni na kifuani.
Tukio hilo baya lilitokea jana saa 10:43 jioni katika viunga vya Mtaa wa Mlandege mjini hapa wakati Padri huyo akitoka ndani ya duka la huduma za mtandao (Internet Cafe).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jeshi hilo linaendelea na msako mkali katika maeneo yote ya mji wa Zanzibar.
“Huyu Padri alikuwa akitoka Internet CafĂ©, ghafla kwa nje alivamiwa na watu watatu ambao walimmwagia maji makali yanayosadikiwa kuwa ni tindikali na kisha kutokomea kusikojulikana.
Kamanda huyo alisema, baada ya tukio hilo Padri huyo alisadiwa na wasamaria wema ambao walimpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu huku taratibu za kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa Muhimbilin jijini Dar es saalam zikiendelea.
Kamanda Mkadam alisema mpaka sasa hakuna mtu aliyeripotiwa kukamatwa juu ya tukio hilo hivyo bado Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa.
“Nimewaagiza maafisa wangu wahakikishe wanawakamata hao waliofanya tukio hilo, pia kwa taarifa nilizokuwa nazo wanaendelea na doria katika maeneo mbalimbali ya mji.
“Tunaendelea kuimarisha na kuongeza askari katika maeneo yote kwa ajili ya kuhakikisha watuhumiwa wanapatikana mara moja,” alieleza kamanda huyo.
Hata hivyo kamanda Mkadam alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zitakazosadia jeshi hilo kuwatia mbaroni wahalifu wa tukio hilo kwa haraka zaidi na kuendelea na uchunguzi wa kina juu ya matukio kama hayo hapa nchini.
Alisema jeshi hilo limeanza uchunguzi wa kina kwa kutumia askari wake waliobobea katika nyanja za upelelezi wa kimataifa ili kuhakikisha wanawapata wahusika wa tukio hilo.
Wakizungumza na MTANZANIA baadhi ya mashuhuda wa liofika katika eneo la tukio, walidai kuwa walishutushwa na kelele za Padri huyo akiwa nje ya duka hilo ndipo walipofika na kumkuta ameanguka chini.
Wananchi hao walilaani vitendo hivyo vya kinyama na uzalilishaji dhidi ya binadamu ambavyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara visiwani humo na kuitaka kuacha kufumbia macho vitendo hivyo.
Tukio hilo limetokea ikiwa umepita mwezi mmoja tangu wasichana wawili raia wa Uingereza kumwagiwa tindikali visiwani humo walipokuwa matembezini katika eneo la Mji Mkongwe.
Wasichana hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 na kuendelea walikuwa wakifanya kazi za kujitolea visiwani humo na kwamba tukio hilo ni la kwanza kufanywa kwa raia wa kigeni visiwani humo.

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts