Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Thursday, September 19, 2013

Tembo Wazidi Kuwa Hatarini Zaidi Mashariki Mwa Afrika

Mvietnamu akamatwa na pembe za kifaru nchini Kenya

Septemba 18, 2013

Maafisa wa usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ya Jomo Kenyatta siku ya Jumanne (tarehe 17 Septemba) walimtia mbaroni mtu mmoja kutoka Vietnam akiwa na pembe tano za kifaru zenye uzito wa kilo 20, Capital FM ya Kenya iliripoti.
Le Manh Cuong, mwenye umri wa miaka 29, alikuwa njiani kutoka Msumbiji kwenda Hong Kong akiwa amebeba pembe za kifaru, ambazo alizitia katika katika mkoba wake wa safari uliokuwa umewekwa vipande vya godoro, alisema msemaji wa Idara ya Wanyamapori ya Kenya (KWS) Paul Muya.
Le alitiwa mbaroni kwa ushirikiano wa timu ya usalama inayoundwa na Kitengo cha Polisi cha Viwanja vya Ndege vya Kenya, maafisa wa Forodha, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya, shirika la ndege la Kenya Airways na KWS. Atafikishwa katika mahakama hya Makadara siku ya Jumatano.
Muya alisema kuwa mwaka huu wageni 39, wakiwemo Wavietnam tisa na Wachina 19, wamekamatwa kwa magendo ya bidhaa harama ya wanyamapori nje ya nchi.
“Mapambano yanaendelea na hatutarudi nyuma hadi tushinde vita dhidi ya ujangili,” alisema.

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts