Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Thursday, September 19, 2013

Somalia inapaswa kufanya nini kuhusu Hassan Dahir Aweys?

Maana ya kufungwa jela -- au kuachiwa huru -- Aweys kwa Somalia

Na Abdi Moalim, Mogadishu

Septemba 18, 2013
Aliyekuwa kiongozi wa al-Shabaab Hassan Dahir Aweys amekuwa katika mahabusu ya serikali ya Somalia kwa miezi zaidi ya miwili, lakini utawala wa rais Hassan Sheikh Mohamud bado haujaweka wazi iwapo unapanga kumfungulia mashtaka mwanamgambo huyo au kumwachia huru.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 77 alijisalimisha kwa Himan na mamlaka za Heeb tarehe 25 Juni baada ya kukimbia mapigano ya kikundi kilichojitenga huko Barawe baina ya vikosi vinavyomtii kamanda wa ngazi ya juu wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane na anayefuatia wa pili kwa kutoa amri Ibrahim al-Afghani, ambaye sasa alishafariki.
Mamlaka za Himan na Heeb kisha zilimkabidhi Aweys kwa mamlaka ya serikali ya Somalia ambazo kwa haraka zilimkamata, kulikochochea wapingaji miongoni mwa wanaomtii kudai aachiwe.
Wakati serikali ya shirikisho ilipotoa kwa mara ya mwisho taarifa kuhusu Aweys mwezi Julai, Mohamud alisema utawala wake ungetangaza uamuzi wake baadaye, pasipo kueleza kwa kina. Kusubiriwa kwa muda mrefu kumesababisha watu kuuliza maswali ya namna serikali ya Somalia inavyokusudia kushikilia uwajibikaji wa wale wanaotuhumiwa kufanya uhalifu dhidi ya raia.

Kubembeleza ugaidi?

Ahlu Sunna wal Jamaa (ASWJ), wanamgambo wanaounga mkono serikali ambao walipigana na Hizbul Islam na al-Shabaab, wanadai kwamba serikali inamfungulia mashtaka Aweys kwa uhalifu alioufanya, alisema Sheikh Omar Abdulkadir, mwenyekiti wa Baraza linaloongoza ASWJ.
"Anapaswa kupelekwa kwenye sheria kushawishi umma wa Somalia kwamba hakuna aliye juu ya sheria kisha kumwadhibu kwa kile kitakachomtia hatiani," aliiambia Sabahi.
Kumwachia huru Aweys kunaweza kudhoofisha jitihada za ususluhishi, Abdulkadir alisema, akielezea wale wanaoshinikiza serikali kumwachia huru Aweys kama vibaraka.
"Kama Aweys anaachiwa, inaweza kusababisha mkanganyiko na kuvunjwa moyo miongoni mwa watu mbalimbali walidhuriwa wakati wa mizozo na kikundi anachoongoza," alisema aliyekuwa mkuu wa Shirika la Upelelzi na Usalama la Somalia (NISA) Ahmed Moalim Fiqi.
Kuchelewa kwa serikali katika kutangaza uamauzi wake kunadhuru jitihada za usuluhishi za kitaifa kwa sababu Wasomali wanaogopa kwamba Aweys anaweza kuachiwa pasipo kupelekwa mahakamani kutokana na shinikizo kutoka kwa wazee wa kimila ambao wanamuunga mmkono, alisema.
Fiqi pia alisema kuachiwa kwa Aweys kungepeleka ishara kwa wanaomtii kwamba serikali haina ukali kwa ugaidi, ikiwahamasisha kuendeleza shughuli zao na hivyo kudhoofisha mamlaka ya serikali.
Serikali inaidhibiti mikoa inayojaribu kufufua sheria na utulivu vitakuwa hatarini kwa wapiganaji wa Aweys, alisema.
Kumwachia huru Aweys bila ya sababu za wazi na za kutosheleza kunaweza kusababisha madhara yasiyorekebishika na kuhatarisha misaada ambayo serikali ya Somalia inapata kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, Fiqi alisema.
"Serikali wahisani zitashindwa kuiamini serikali ya Somalia, hasa kuhusu jinsi itakavyoshughulika na viongozi na wanachama wa al-Shabaab baada ya kukamatwa na serikali," alisema. "[Hili pia] litaleta mashaka kuhusu mipango ya serikali katika kupambana na ugaidi, ambako kutasimamisha misaada inayohusiana na masuala hayo."

Historia ndefu ya msimamo mkali

Mapema katika miaka 1990, Aweys alijiunga na kuwa kiongozi wa al-Itihaad al-Islamiya (AIAI), kundi lililokuwa kwa sehemu likifadhiliwa na Osama bin Laden na kuhusishwa na mashambulizi kadhaa ya kigaidi katika Pembe ya Afrika.
Chini ya uongozi wake, AIAI alihusika katika mapigano kadhaa ili kupata udhibiti wa maeneo ya Somalia, ikiwa ni pamoja na mapigano ya Saliid huko Nugal, moja ya mapambano makali katika historia ya mkoa, kwa mujibu wa wazee wa kimila waliozungumza na Sabahi.
Watu kama Aweys wanaohusika na mauaji ya raia wa Somalia wanapaswa kuwajibishwa, alisema Said Dahir, mzee wa kimila huko Mogadishu.
"Tunaomba kwamba ashitakiwe kwa uhalifu alioufanya dhidi ya taifa. Tunapinga kuachiwa kwake bila ya kukabiliwa na mashtaka yoyote," Dahir alisema.
Dahir Irro, aliyefanya kazi kama mbunge akiwakilisha Puntland chini ya serikali ya shirikisho ya mpito, pia alisema Aweys lazima awajibike kwa makosa yake ya nyuma na hapaswi kutolewa kifungoni.
Kama sehemu ya AIAI, na baadaye Uislamu wa Hizbul na al-Shabaab, Aweys alisaidia kukua kwa msimamo mkali Somalia, alisema.
"Aweys alikuwa sehemu ya vikundi vya kupingana na amani, chanzo cha migogoro [ ya Somalia], na ambaye alieneza itikadi ya kupotosha ambayo imeangamiza maisha ya raia," Irro aliiambia Sabahi.

Kuchagua amani

Hata hivyo, Aweys bado anaweza kutimiza wajibu katika kuleta amani kwa Somalia, kwa mujibu wa Robert Young Pelton, mwandishi wa habari wa Canada na mtunzi ambaye ameandika kuhusu Somalia.
"Amani ya Somalia wakati wote imejikita katika mazungumzo kati ya pande zilizohusika katika mgogoro," alisema.
Vita hiyo ya Awey na wananchi imeathiri wajibu wake wa kisiasa na kupunguza ushawishi wake wa awali kwa umma wa Somalia, na imesababisha yeye kuwa mlengwa kwa serikali za kigeni, alisema Pelton.
Hata hivyo, kushiriki katika mazungumzo na Awey kutahamasisha wote wanaounga mkono mawazo yake ya msimamo mkali kuwa na kasoro kutoka kwa al -Shabaab na kujiunga na serikali, alisema Pelton.
Hizbul Islam alitangaza Jumatatu (tarehe 16) kwamba amesimama kutumia vurugu na badala yake atasaidia amani na mapatano nchini Somalia.
"Baada ya kukosa mazungumzo ndani ya shirika, Hizbul Islam alikiri itasimamisha mapigano na kuchukua njia ya amani," alisema msemaji Sheikh Mohamed Moalim. Tutakuwa kundi la kisiasa badala ya kikundi cha vita."
Kikundi pia kilishutumu wenye msimamo mkali, wakisema inafanyika kinyume cha dini, na imeeneza wito wa kumuachia Aweys.
Kwa upande wake mzee wa kimila wa Galowe Khalif AW Ali alisema kama Aweys anatubu kweli -- bila msuguano kutoka kwa serikali au wadau wengine -- anapaswa kuruhusiwa kurejea katika jamii yake.
"Anapaswa kuwa na mijadala na ufafanuzi wa lengo lake halisi," Ali aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba, ukimya wa Awey haukusaidia kuboresha wazo la umma kuhusiana na kesi yake.
Taarifa ya nyongeza ya Ali Adam huko Mogadishu na Hussein huko Garowe
Swali: Unadhani serikali ya Somalia inapaswa kufanya nini kuhusu Hassan Dahir Aweys? Toa maoni yako katika maoni hapo chini.
Chanzo: Sabahionline 

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts