Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Thursday, September 12, 2013

Tunawajengea Watoto Tabia ya Kuishi Kwa Makosa

Ulinzi mkali mtihani darasa la saba

Sura za Habari Hii
Ulinzi mkali mtihani darasa la saba
Maoni ya wanafunzi
Habari Yote
WANAFUNZI wa darasa la saba jana walianza kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi, huku katika Jiji la Dar es Salaam ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa katika shule mbalimbali. Tofauti na miaka ya nyuma, ambapo ulinzi umekuwa ukifanywa na askari wa kawaida, lakini mwaka huu ulinzi umeimarishwa kwa kuwapo Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
Ulinzi huo mkali ulionekana zaidi katika shule za msingi za Serikali, huku katika shule zinazomilikiwa na watu binafsi, kukiwa na ulinzi wa kawaida.
MTANZANIA ilitembelea katika shule mbalimbali jijini Dar es Salaam, ikiwamo Shule ya Dk. Omari Ali Juma, Karume, Mianzini, Mburahati, Mapinduzi, Buguruni Viziwi, Mtakatifu Agostino, Atlas, Mtakuja, Kombo, Mugabe, Al-hikma, Hekima, Buguruni ‘A’ na German Rutihinda.
Mlinzi wa Shule ya Msingi Dk. Omari Ali Juma ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema: “Hali ya ulinzi ni kali sana, tofauti na miaka yote.
“Miaka iliyopita kulikuwa na askari polisi na wasimamizi, lakini leo wapo hadi FFU, sisi wenyewe haturuhusiwi kusogea maeneo ya madarasa, zamani haikuwa hivi,” alisema mlinzi huyo.
Baadhi ya shule mageti yake yalifungwa na wanafunzi hawakuruhusiwa kutoka nje ya shule kipindi cha mapumziko.
Wakati kukiwa na ulinzi huo, baadhi ya shule zilizopo karibu na maeneo ya barabara ikiwamo Shule ya Msingi Mianzini iliyopo maeneo ya Mburahati, Kombo na Mtakuja zilizopo Vingunguti zilitawaliwa na kelele nyingi hususani za pikipiki na muziki.
Muda mfupi baada ya waandishi kuondoka katika lango la shule hiyo, mlinzi huyo aliondoka katika eneo lake la kazi na kwenda kuwaamuru wafanyabiashara wa maduka yaliyopo karibu na shule hiyo kuzima muziki wao.

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts