ICC yaiweka kesi ya Ruto kuwa kikao cha faragha kwa ajili ya usalama wa mashahidi
Septemba 20, 2013
Jaji anayesimamia kesi ya Makamu Rais wa Kenya William Ruto katika
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ameamua kwamba shahidi wa kwanza
wa upande wa mashtaka atatoa ushahidi wake uliobakia kwa kamera katika
kikao cha faragha, liliripoti gazeti la Daily Nation la Kenya siku ya
Alhamisi (tarehe 19 Septemba).
Baada ya vyombo vya habari vya nchini Kenya na wanablogu wa huko kuchapisha jina na picha zinazoweza kuwa za shahidi huyo, mahakama hiyo ilionya dhidi ya kuweka hadharani utambulisho wa mashahidi wanaolindwa.
Wakili wa Ruto, Karim Khan, alipinga hatua hiyo. "Hakuna hatari yoyote kwa shahidi huyo. Tayari yuko kwenye ulinzi wa wahanga na mashahidi," alisema, akiongeza kwamba picha zilizochapishwa si za shahidi huyo.
Wakati huo huo, kiti cha rais wa ICC kimekataa maombi ya Umoja wa Afrika wa kusitisha kesi ya Ruto hadi pale ombi lake la rufaa ya kuzihamishia kesi yake na ya Rais Uhuru Kenyatta nchini Kenya yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi, kikiongeza kwamba ni majaji wanaosikiliza kesi hiyo ndio wanaoweza kutoa maamuzi hayo.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya watafanya mkutano maalum wa kilele mwezi ujao mjini Addis Ababa huku kukizidi kuongezeka kwa upinzani kwenye eneo hilo dhidi ya kesi hizo, liliripoti shirika la habari la AFP. Umoja wa Afrika umeituhumu ICC kwa kuwalenga Waafirka tu kwenye mashtaka yake.
Mkutano huo wa kilele "utakuwa ni wa kufuatilia uamuzi waliochukua mwezi Mei... ambapo waliiomba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kufanya uwezekano wa kuipa Kenya fursa ya kuwachunguza na kuwahukumu watuhumiwa," alisema naibu mkuu wa halmashauri ya Umoja wa Afrika, Erastus Mwencha.
Chanzo; Sabahionline

No comments:
Post a Comment