Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Monday, September 23, 2013

Hali ya Fukwe za Moghadishu

Waokoaji maisha waleta matokeo ya haraka katika ufukwe wa Mogadishu

Na Dahir Jibril, Mogadishu

Uongozi wa Benadir umewapa mafunzo na kupeleka timu ya waokoaji maisha ili kuokoa watu wasizame katika Ufukwe wa Lido huko Mogadishu.
  • Mvulana mdogo akicheza katika katika wimbi kwenye Ufukwe wa Lido wakati watu wakisherehekea Eid al-Fitr hapo tarehe 8 Agosti. Waokoaji maisha sasa wanalinda ufukwe ili kuzuia watoto na watu wengine wasisombwe na maji. [Na Tobin Jones/AU-UN IST/AFP] Mvulana mdogo akicheza katika katika wimbi kwenye Ufukwe wa Lido wakati watu wakisherehekea Eid al-Fitr hapo tarehe 8 Agosti. Waokoaji maisha sasa wanalinda ufukwe ili kuzuia watoto na watu wengine wasisombwe na maji. [Na Tobin Jones/AU-UN IST/AFP]
Tangu timu ya waokoaji maisha 15 ilipoanza tarehe 1 Septemba ikiwa na idadi ya boti tano za uokozi, imeokoa watu kumi, wakiwemo watoto wawili, alisema Mkuu wa Wilaya ya Abdiaziz, Abdullahi Hussein Hassan.
"Nimekuwa nikifanya kazi kuanzisha boti hizi za doria kwa sasa ili kuwaokoa watu wa Somalia, kwa vile karibuni kumekuwa na ongezeko la vijana wa Somalia waliojeruhiwa katika bahari," aliiambia Sabahi. '
Kituo cha afya cha dharura sasa kinafanya kazi katika Ufukwe wa Lido ili kutoa huduma za afya kwa watu wanaojeruhiwa wakiwa wanaogelea au kusafiri baharini, alisema.
"Mara nyengine vijana hufanya safari za kujifurahisha baharini, lakini wanaweza kurejea nyumbani kwa mashaka bada ya mmoj a wa marafiki zao kuchukuliwa na maji baharini," Hassan alisema. "Sasa tunafanya kazi kwa juhudi ili kuepusha hilo."
"Kazi ya boti hizi sio tu kuwaokoa watu; pia zinawazuia vijana wasiogelee katika maeneo ya mbali sana na ufukwe kwa kuwataka kurejea nyuma kama njia ya kuweza kuwaangalia waogeleaji," alisema.
Hassan aliwataka wafanyabiashara wa Somalia kusaidia katika upatikanaji wa boti zaidi za uokoaji ili waokoaji waweze kutoa msaada mzuri zaidi, hasa wakati wa mawimbi kubwa.

Kupunguza hofu

Wamiliki wa mikahawa katika Ufukwe wa Lido wanahamu ya kuwasaidia waokoaji maisha, alisema Mohamed Abdullahi Ali, meneja wa Lido Bar.
"Tunakaribisha kwa hamu vijana waliopewa mafunzo kama waokoaji maisha ili kuokoa watu wanaokuja kuogelea katika Ufukwe wa Lido," aliiambia Sabahi. "Mpango wetu wa haraka haraka ni kukutana na watu hawa wanaoshughulika na juhudi hizi ili tuweze kushauriana nao juu ya namna ya kuwasaidia."
Shamso Omar, mwenye umri wa miaka 39 na mama wa watoto sita wanaoishi katika wilaya ya Abdiaziz, alielezea kufarijika kwake na shukrani kwa boti za kuokoa maisha zinazofanya doria katika maji ya ufukweni.
"Kwa moyo mmoja ninakaribisha juhudi [za uongozi wa Benadir] katika [kuanzisha] kikundi hiki ambacho kinawaokoa watoto wetu katika Ufukwe wa Lido," aliiambia Sabahi. "Hatuwezi kuwazuia watoto na vijana wasiende ufukweni wakati wa mapumziko ya shule. Nimefurahi kwamba hofu yangu katika hilo imepungua."
Mkaazi wa Wilaya ya Hamar Weyne Faisal Hassan Yare, mwenye umri wa miaka 27, alisema aliwaona watoto wadogo na vijana ambao sio waogeleaji wazuri wakisombwa na mawimbi na mikondo ya maji "mara nyingi".
"Nilihuzunishwa sana," Yare aliiambia Sabahi. "Ujuzi wangu wa kuogelea sio mzuri kuweza kumuokoa yeyote, lakini nimeshirikia katika uokoaji wa watoto mara kadhaa. Nina hakika watu wanaweza kuokolewa na boti hizi."
"Ni rahisi kwa bahari kusomba mtu lakini sio rahisi kumuokoa mtu," Yare alisema. "Ningependa kuwashauri [waokoaji] kuwa na tahadhari ya ziada kuhusu usalama wao, na vijana wadogo wasiruhusiwe kuogelea mbali na ufukwe."
Chanzo: Sabahionline

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts