Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Saturday, September 14, 2013

Wahamiaji Haramu Kujificha Kwenye Majumba ya Ibada!

Wahamiaji haramu: Msako waingia makanisani

*Mchungaji, waumini sita watiwa mbaroni
*Wageuza makanisa maficho, Uhamiaji yahaha

MSAKO wa wahamiaji haramu umeingia katika sura mpya, baada ya Idara Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, kuanzisha msako mkali katika nyumba za ibada. Kabla ya kuanzisha msako huo, kumekuwa na taarifa nyingi kuwa baadhi ya makanisa, hasa ya Pentekoste, yanadaiwa kuhifadhi wahamiaji haramu kinyume cha sheria.
Katika msako huo, idara hiyo imemkamata Mchungaji wa Kanisa la Kimataifa la Life Changer Chapel, lililopo Sinza ‘E’, Grace Dangana Omotok, ambaye ni raia wa Nigeria.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Hokororo, alisema Mchungaji Grace alikamatwa baada ya kukiuka masharti ya kibali chake ambacho hakimruhusu kumuingiza raia yeyote nchini.
Alisema mchungaji huyo, alikamatwa Jumatano wiki hii, akiwa na raia wengine sita ambao wanaishi nchini kinyume cha sheria.
“Mchungaji Grace ana kibali Class C ambacho hakimruhusu kuingiza raia wa nchi nyingine.
“Tumekuwa na msako mkali, katika kanisa lake tumewakamata wahamiaji haramu sita ambao ni raia wa Nigeria na hatujui aliwaingizaje, tunaendelea na mahojiano nao ili kujua walivyoingia nchini.”
Alisema Idara ya Uhamiaji haina mpango wa kukutana na viongozi wa dini kuzungumzia uendeshaji wa operesheni hiyo, kwa sababu baadhi ya viongozi si waaminifu.
“Hatufikiri kukutana na kiongozi yeyote wa dini, tutaendeleza msako hadi Jiji la Dar es Salaam liwe na wahamiaji halali tu.
“Mfano wa mchungaji huyu, umeonyesha picha ya wazi kuwa viongozi wa dini si waaminifu, hatuna sababu ya kuzungumza nao, unadhani watatuambia nini zaidi ya kujitetea?
“Kama kiongozi wa dini alifanya hivyo kwa kupitiwa, aliposikia kuna msako kwanini asijisalimishe na watu wake?” alihoji Hokororo.
Hata hivyo, alisema nguvu kubwa hivi sasa itaelekezwa kwenye nyumba za ibada na kwenye saluni mbalimbali jijini humo, maeneo ambayo yanadaiwa kuwa na wahamiaji haramu wengi.
“Tukipata taarifa kuwa kuna kanisa linawahifadhi wahamiaji haramu tutafuatilia, huu msako ni endelevu, hata wakijificha wapi tutawakamata tu,” alisisitiza ofisa huyo.
Alisema wahamiaji haramu ambao watajisalimisha wenyewe watapewa nafasi ya kusikilizwa kuliko watakaokamatwa katika msako.
Inadaiwa makanisa mengi yanahifadhi wahamiaji haramu kwa kigezo cha kutangaza neno la Mungu, wakiamini kuwa maeneo hayo ni salama.
Wahamiaji haramu 465 kutoka mataifa mbalimbali, walikamatwa jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Taarifa za idara hiyo, zinasema kuwa idadi kubwa ya wahamiaji waliokamatwa ni vijana.
Msako huo, ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete, alilolitoa Julai 26, mwaka huu, mkoani Kagera, ambapo aliwataka wahamiaji haramu kuondoka nchini kwa hiari yao.
Wahamiaji kutoka mataifa 17, walikamatwa katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam.

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts