Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Wednesday, October 9, 2013

DKT. MAGUFULI AWABANA WABISHI!


kitaifa image DKT. MAGUFULI AWAGOMEA WENYE MABASI, MALORI Wednesday, October 9 2013, 8 : 1 Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli amesema hawezi kubadili i uamuzi wake wa kufuta msamaha wa tozo kwenye mizani kwa uzito wa magari uliozidi asilimia tano ya ule unaokubaliwa kisheria licha ya wamiliki wa malori na mabasi kusitisha huduma. Dkt. Magufuli aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, hamzuii mtu kusitisha huduma katika barabara ambazo amepewa jukumu la kuzisimamia. Alisema Wizara imechukua jukumu la kulipeleka suala hilo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova ili waweze kuchukua hatua. Aliongeza kuwa, pia amewasiliana na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe juu ya uamuzi wa kufuta msamaha huo.“Nitaendelea kusimamia uamuzi huu ambao upo kwa mujibu wa sheria namba 30 ya mwaka 1973 ya Usalama Barabarani iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2001. “Sheria hii ina kifungu kinachowapa fursa wamiliki wa malori kufungua kesi mahakamani kupinga uamuzi huu badala ya kugoma na kuzuia haki ya wengine kutumia barabara, waende mahakamani wakapambane na mawakili wa Serikali,” alisema Dkt. Magufuli. Aliongeza kuwa, hatua nyingine wanayoweza kuchu kua ni kumwandikia barua Waziri mwenye dhamana vinginevyo wapeleke hoja hiyo bungeni kuomba marekebisho ya sheria hiyo. Alisema ana taarifa kwamba mgomo huo unachochewa na mfanyabiashara mmoja ambaye yupo tayari kumtaja kama atakwenda mahakamani.“Uamuzi huu umekuja baada ya kurekebisha matatizo yaliyopo katika vituo vya mizani ambapo asilimia 65 ya wafanyakazi walikuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa hivyo tayari wamefukuzwa kazi na kuajiriwa wengi wapya,” alisema. Kwa upande wake, Kamishna Kova alisema jeshi hilo limejipanga kulinda usalama ili watumiaji wa barabara wasipate usumbufu ambapo kabla hawajachukua hatua za kisheria ni vema vyombo vinavyosimamia usafirishaji vikachukua hatua. Wakati huo huo, Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani (TABOA), kimesema kitasitisha kutoa huduma kuanzia leo baada ya kukosekama mwafaka na Serikali. Akizungumza na Majira, Katibu Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu alisema hadi saa 11 jioni, hakukuwa na mwafaka wa jambo hilo; hivyo hawatatoa huduma hadi madai yao yasikilizwe. Alisema msamaha huo umedumu muda mrefu lakini kitendo cha Dkt. Magufuli kuchukua uamuzi huo peke yake bila kuwashirikisha hakikubaliki na ndio sababu kubwa ya mgogoro uliopo. Alisema ni jambo la ajabu kuona suala hilo linapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kulipatia ufumbuzi wakati wahusika wakuu wapo na wana uwezo wa kuamua mara moja kwani jambo hilo ni muhimu. Awali, Serikali ilitangaza kuwa magari yote yatakayobainika kuwa na uzito uliozidi lakini upo ndani ya asilimia tano ya ule unaokubaliwa kisheria, watatakiwa kupunguza mzigo, kupanga mzigo au kulipia uzito uliozidi mara nne ya tozo ya kawaida. Chanzo: Majira

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts