Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Wednesday, October 9, 2013

WAPINZANI WAZIDI KUJIIMARISHA!


gory: kitaifa image CHADEMA, CUF, NCCR WAKWAMA Wednesday, October 9 2013, 8 : 3 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, haitajadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya mwaka 2013, uliopitishwa katika Bunge la 12, Mjini Dodoma. Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Bw. Tundu Lissu, alisema kwa kuwa suala hilo halipo kwenye ratiba, kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa hoja zao zinazungumzika, si jambo linalowezekana. Alisema mswada huo ulipaswa kuwepo kwenye ratiba lakini haupo, hivyo ni wazi kuwa kauli ya Rais Kikwete haina ukweli kama alivyoahidi katika hotuba yake ya Septemba mwaka huu. Aliongeza kuwa, kamati hiyo itakwenda Zanzibar kuchukua maoni ya wananchi kuhusu kura ya maoni na marekebisho ya sheria mbalimbali. Bw. Lissu alisema kamati itaondoka Dar es Salaam kesho na itakaa Zanzibar siku tatu ambapo siku mbili zitatumika kukusanya maoni ya watu mbalimbali na siku moja ya marekebisho ya sheria. “Miswada mbalimbali ukiwemo wa Sheria ya Vyombo vya Habari itajadiliwa, wadau wataanza kutoa maoni yao kuanzia Oktoba 14 mwaka huu,” alisema. Alisema Mswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari umeongezewa makali, faini pamoja na adhabu ya kufungiwa vyombo husika. Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye alikuwa Mwenyekiti katika kamati hiyo, Bw. William Ngeleja, alisema kamati hiyo itajadili Miswada miwili ambayo ni ya kura ya maoni na marekebisho ya sheria mbalimbali. “Kamati itapokea maelezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu Mswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali mwaka 2013 na maelezo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Mswada wa Sheria ya Kura ya Maoni ya mwaka 2013,” alisema. Chanzo: Majira.

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts