MAREKANI KUWAREJESHA WAFANYAKAZI KAZINI
Wizara ya ulinzi ya marekani imesema itawarejesha kazini wafanyakazi wake wengi walioachishwa kazi kwa muda, wakati shughuli za nchi hiyo zikiendelea kufungwa bila dalili za kumalizika mkwamo huo.
Akitoa hotuba yake ya kila wiki kwa taifa kupitia redio, rais wa marekani, barack obama, amewataka wabunge wa republican kupiga kura ya kuidhinisha bajeti ili kuiwezesha serikali kuendelea na shughuli zake.
Hata hivyo, viongozi wa republican wamedai kuwa rais obama ndiye anayestahili kulaumiwa kwa mkwamo huo, kwa sababu ya kutotaka mashauriano.
Waziri wa ulinzi, chuck hagel, ametangaza kuwa wengi wa wafanyakazi 400,000 wa wizara ya ulinzi watarejeshwa kazini wiki hii. Bw. hagel amesema mawakili wa wizara yake wamebaini kuwa sheria inawaruhusu wafanyakazi "ambao majukumu yao yanachangia morali, ustawi, uwezo na hali ya kuwa tayari kwa watoaji huduma" kutohusishwa na hali hiyo ya kufungwa kwa shughuli za serikali.
Serikali ya marekani mapema wiki iliyopita ilifunga operesheni zake zote isipokuwa zile muhimu wakati wabunge wa chama cha republican walipokataa kuidhinisha fedha za matumizi ya serikali bila ya kwanza kuchelewesha au kusitisha fedha za sheria mpya ya huduma za matibabu, maarufu kama obamacare.
No comments:
Post a Comment