Pageshttps://www.insidehighered.com/views/2020/02/05/why-institutions-should-continue-support-their

Graduation

Graduation
From left: Jumanne Hussein, Dr.Suru, Mzee Gantala, Dr. Masoud during the graduation ceremony held on 26th November, 2015 at Chimwaga Hall, Dodoma

Wednesday, October 9, 2013

POLISI YAKAMATA WATU WASIOJULIKANA WAKIFANYA MAZOEZI MSITUNI!


MBARONI ‘WAKIJIPIKA’ KIJESHI Monday, October 7 2013, 21 : 51 Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, limewatia mbaroni watu 11 wakiwa katika Mlima wa Makolionga, Wilaya ya Nanyumbu, mkoani humo wakiwa kwenye mafunzo ya msituni. Wakiwa katika maficho hayo, watuhumiwa hao walikamatwa na CD zipatazo 25 zenye mafunzo mbalimbali baadhi yakiwemo ya Al Shabaab, mauaji ya Osama Bin Laden, Zindukeni Zanzibar, kuandaa majeshi, mauaji ya IdiAmin na Mogadishu Sniper. Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Zelothe Stephen, alisema pamoja na CD hizo, watuhumiwa walikuwa na zana zingine pamoja na vyakula. Vitu hivyo ni DVD player moja, Solar panel moja (watts 30), mapanga mawili, visu viwili, tochi moja, betri moja ya pikipiki, simu za viganjani tano, vyombo mbalimbali vya chakula, jiko moja la mkaa, jiko la mafuta ya taa na taa moja ya chemli. Vingine ni baiskeli tatu, ndoo nne za maji, vitabu mbalimbali vya dini ya Kiislamu, unga wa mahindi kilo 50, mbaazi kiroba kimoja (kilogramu 50), mahindi viroba vitatu (kilogramu 150) pamoja na virago vya kulalia. Kamanda Stephen alisema vitu vingine walivyokutwa navyo ni mfuko wa kijani unaosadikiwa wa kijeshi (Kit bag) wenye nembo ya nanga ya meli yenye mistari kulia na kushoto pamoja na nyoka katikati. Aliwataja watu hao kuwa ni Mohamed Makande Matete (39), mkazi wa Kijiji cha Sengenye ambaye ndiye kiongozi wa kundi hilo, Hassan Omari Ajili (39), mkazi wa Nalunyu, Rashid Ismail (27) na Abdallah Yusuph Hamis (32), wote wakazi wa Likokona. Wengine ni Salum Bakari Wadi (38), Ramadhan Adamu Rajabu (26), Fadhil Adamu Rajabu (20), Abbas Muhdini (32), Isamili Chande (18), Said Mawazo (21) na Issa Abed, wote wakazi wa Likokona. “Watuhumiwa wote tayari wamefikishwa mahakamani na wakati huo huo Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa kina kuhusu tukio hili ambalo si la kawaida. “Tunasaidiwa na Makao Makuu ya Polisi na mikoa mingine ili kuwanasa watu wote waliotajwa kuhusishwa na tukio hilo la mafunzo ya kutisha na hatari,” alisema. Alitoa wito kwa wananchi wote wenye taarifa inayohusiana na tukio la aina hiyo, watoe taarifa mapema iwezekanavyo ili watu hao wakamatwe na sheria kuchukuliwa mkondo wake. Chanzo: Majira

No comments:

Followers

UNGANA NA ULIMWENGU WA SELFIE

Habari Bayana

News Alerts